Safari ya shirika la WaterAid Tanzania kujumuisha ubunifu na teknolojia katika miradi ya maji ili kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama Tanzania

6 min read
Mkurugenzi Mkaazi wa WaterAid Tanzania akimuelekeza Naibu Waziri wa Maji, Mary Prisca Mahundi namna teknolojia ya kuchuja  maji inavyofanya kazi alipotembelea eneo la mradi Arusha
Image: WaterAid/Neema Kimaro

Kote ulimwenguni kila ifikapo tarehe 22 Machi kila mwaka, tunaadhimisha siku ya maji duniani. Kila mwaka hubeba kauli mbiu tofauti na mwaka huu ni “Maji ya ardhini: kufanya yale yasiyoonekana yaonekane” Ni nini kinakuja akilini unapofikiria kuhusu maji ya ardhini? Je, unafikiri ni salama na safi au machafu? Ukweli ni kwamba maji ya ardhini yanaweza kuwa safi na salama kwa wanadamu endapo tu kutatumika ubunifu na teknolojia ili kufanya chanzo cha maji kisichooekana kuonekana na kuwa na maji safi na salama.

CHANGAMOTO ILIYOPO

Nchini Tanzania watu 2 kati ya 5 hawana maji safi karibu na nyumbani. Wanawake na wasichana hutembea umbali mrefu kutafuta maji ambayo mara nyingi huwafanya kuwa wagonjwa. Nyumba, shule na vituo vya afya vingi nchini vinakosa huduma za msingi za maji safi. Chanzo chochote cha maji kinaweza kuwa safi lakini si salama, na kwa hilo ina maana kwamba maji yanaweza kuwa na chumvi nyingi na kwa baadhi ya maeneo ya Tanzania, floridi ni nyingi. Tanzania iko katika hatari kubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa. Joto linaongezeka, na ukame ni wa mara kwa mara. Visima vinakauka, na uchafuzi wa maji ya bahari unafanya maji ya chini ya ardhi kutokuwa salama kwa kunywa. Watu katika jamii zilizo na kipato duni ndio huathirika zaidi.

LENGO LETU KATIKA SEKTA

Tangu mwaka 1983, WaterAid Tanzania shirika la kimataifa lisilo la kimaslahi limeazimia kufanya maji safi, vyoo bora na usafi wa mazingira kuwa jambo la kawaida kwa kila mtu, kila mahali ulimwenguni kote. Ni kwa kuyapa kipaumbele mambo haya matatu muhimu kwa njia za kudumu tu ndipo watu wanaweza kubadilisha maisha yao.. Kama shirika, Tumepitia mageuzi mbalimbali katika kuhakikisha tunawafkia watanzania wengi kadiri inavyowezekana, sio tu kwa kuwapatia maji safi, bali na salama pia.

KUJUMUISHA TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

Unaweza kujiuliza tulifanyaje ili maji ya chini ya ardhi yasiyoonekana, yakaweza kuonekana kwa kutumia teknolojia na uvumbuzi? Kwa kutumia teknolojia ya Reverse Osmosis ili kuondoa Floridi kutoka kwenye maji ya chini ya ardhi, kuyafanya kuwa safi na salama kwa ubunifu ikiwa ni pamoja na kuweka mita za maji za kielektroniki ya malipo ya kabla; pampu mseto za kusukuma maji (muunganiko wa nishati ya jua na umeme), WaterAid Tanzania imefanikiwa kuokoa watu 30,000 kwenye hatari ya kupata magonjwa ya meno ya mifupa yatokanayo na floridi katika maji katika vijiji vitano mkoa wa Arusha.

Mfumo wa malipo ya awali katika huduma za maji una faida nyingi ikiwemo uwezo wa kupata maji muda wowote wa siku na unaondoa haja ya kuajiri msimamizi wa vituo vya maji inayopelekea kuondoa mianya ya rushwa iwapo msimamizi huyo atakua akisimamia upokeaji wa fedha za manunuzi ya maji. Vituo vya maji vyenye mfumo huu vilivyoko Kijiji cha sangara wilaya ya Babati vinawezesha jamii kuweza kupata maji kwa uharaka na urahisi zaidi. Kwa sasa wakazi wa Sangara hawatumii muda mrefu kutafuta maji na kupitia mradi huu, tumeweza kufikia shule 1 na kaya 358 Kabla ya mradi huu, tulikua na tatizo la umbali wa kituo cha maji ambapo kilikua kilomita 1.5 kutoka nyumbani. Hivi sasa nikiamka asubuhi natembea dakika moja Napata maji safi na salama. Zamani ilikua unaweza ukafika katika kituo cha maji lakini mpokea fedha hayupo lakini sasa tunaweza kupata maji muda wowote ule, nimeupenda sana huu mfumo mpya wa malipo ya awali.

 Pia, Kupitia mpango wa maji uliopo ambao kwa sasa unasambaza maji kwa jamii ya Basuto ya Hanang Manyara, hutoka ziwani bila matibabu yoyote na kutumiwa na wanajamii. Baadaye yalipimwa na kubaini kuwa kiwango cha floridi ni cha juu (juu ya viwango vya Shirika la Afya Duniani) katika usambazaji wa maji hivyo kuhitaji kuchujwa ili kufanya maji kuwa salama kwa matumizi ya binadamu. Mbinu ya kuchuja majii liyotambuliwa kama Nalgonda ambapo kemikali zinatumika kuondoa floridi na chembe chembe nyingine kutoka kwenye maji ili kuweka usafi na salama kwa matumizi ya binadamu kwa watu 14,000.

USHIRIKA

Kwa miaka mitano, WaterAid Tanzania imeweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maji kwa kushirikiana na washirika wa serikali na washirika wa maendeleo kama vile Ofisi ya Maendeleo ya Jumuiya ya madola (FCDO), Kampuni ya Bia ya Serengeti, Habitat for Humanity, Coca-Cola, n.k. Pia kujenga ubia na mitandao yenye nguvu zaidi ili kuimarisha uratibu, kuimarisha ujuzi, uwajibikaji na kushirikishiana na wadau wa maendeleo kupitia Tawala za mikoa na serikali za mitaa,, kitaifa na kimataifa. Kupitia ushirika huo, tumeweza kufikia watu 184,776 kwa maji safi na salama na kufungua vitio vya maji vijijini katika kipindi cha miaka 5 (2016- 2021) “Mpango huu umeleta mabadiliko makubwa ya kitabia kwa jamii na watoto ambao wamefikiwa na kampeni kwani watoto wengi hawakuwa na mikono lakini sasa kwa kampeni hii, vifaa vya unawaji mikono, na matukio ya kijamii, tuna uhakika wa mabadiliko. Tayari tumeona kwenye kaya nyingi na wafanyabishara wana maji safi na salama” Issa Sumari,Afisa Afya - Arusha DC

NINI ZAIDI

Kupitia utoaji wa huduma za maji safi, vyoo bora na siha binafsi na usimamizi wa rasilimali za maji, upunguzaji wa hatari za maafa na usimamizi ili kuongeza utayari wa kukabiliana na matishio ya usalama wa maji na huduma za maji, vyoo bora na siha binafsi.. Mipango/Programu zetu ya kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa zimekua ikifanya kazi na jamii na serikali za mitaa ili kuanzisha uwezekano wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na majanga kupitia teknolojia,ubunifu na usimamizi endelevu. WaterAid Tanzania ina mpango wa kuendeleza miradi iliyoko kwa kuijumuisha na mipango mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kufikia jamii nyingi zaidi nchini hasa maeneo ya Singida na Dodoma kwasababu kama ilivyo Babati, maeneo haya yameathirika sana na mabadiliko ya tabia nchi. Ambayo hupelekea ukosekanaji wa maji safi na salama. WaterAid Tanzania inatumia ushahidi kutoka kwa utafiti, uzoefu wa kiutendaji, na kufanya kazi na washirika wengine wa sekta ili kushawishi serikali na watoa huduma, kudumisha uwajibikaji katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja na mashirika ya uangalizi ya kitaifa na ya ndani. Tunaisaidia serikali ya Tanzania kwa kutoa mafunzo ya kitaalamu na msaada kwa mamlaka za maji. Tunatumia uzoefu wetu kupeleka maji safi hadi maeneo ya mbali, vijijini ili kuasaidia wengine kufanya vivyo hivyo. Na tunatumia kila kitu tunachojifunza wakati wa miradi yetu kushawishi mabadiliko sera katika ngazi ya taifa.

KUFIKIA KILA MTU KILA MAHALI

Washirika wetu ni sehemu muhimu ya WaterAid na ni muhimu kwa kila kitu tunachofanya pamoja. Tunaamini kwamba bila maji safi, vyoo bora na siha binafsi watu hawawezi kuishi maisha yenye utu na afya bora. Tunajua kutokana na uzoefu kwamba kwa haya mambo matatu,binadamu anaweza kuondokana na umasikini na kubadilisha maisha yake. Katika ulimwengu wenye vipaumbele vingi vilivyoshindani, tunabaki thabiti kushughulikia mambo haya matatu muhimu kwa sababu yanabadilisha maisha ya watu. Tunatarajia kufanya kazi na washirika ambao sio tu wanaleta ujuzi sahihi lakini pia maono na maadili.

Tutaendelea kubuni masuluhisho mahiri ya vitendo ambayo yanashikamana na yanaweza kutumika hadi viwango vya kitaifa na kimataifa. Kati yetu, tunayo dhamira, uzoefu, ustadi wa kubadilisha maisha ya mamilioni- hadi kila mtu kila mahali apate kile ambacho wengi wetu hukichukilia kuwa cha kawaida.

Mkurugenzi wetu nchini Bi Anna Mzinga anasema; “Katika dunia yenye vipaumbele vingi vinavyoshindana, WaterAid Tanzania inasalia kuangazia kwa dhati kushughulikia mambo haya matatu muhimu kwa sababu yanabadilisha maisha. Kufanikisha lengo la 6 la maendeleo endelevu ifikapo 2030 kutachukua zaidi ya ufadhili- kunahitaji mbinu mpya, ustadi mkubwa na uvumbuzi wa kweli"